KUVIMBA KWA KORODANI NA MAUMIVU YA KORODANI SABABU NA TIBA

MAUMIVU NA KUVIMBA KWA KORODANI ZA MWANAUME Ni ugonjwa unaoathiri korodani na kuifanya ivimbe, ugonjwa huu unaweza kusababishwa na bacteria au virusi. Kutokana na maambukizi ya vimelea hivi bacteria na virusi huweza kupelekea kuathirika kwa korodani moja au zote mbili kwa wakati mmoja. Lakini kabla ya kwenda mbali zaidi ni vizuri kukumbuka kwamba korodani kazi yake kubwa ni kuzalisha mbegu za kiume. Chanzo cha tatizo hili · Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni aina ya virusi vijulikanvyo kama ‘mups virus,’ kwa hiyo virusi hawa endapo watashambulia korodani husababisha korodani kuvimba na kupunguza utendaji kazi wake. · Maambukizi yanayotokana na vimelea (bacteria) inawezekana ni vimelea wanaosababisha tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) na magonjwa mengine ya zinaa kama Kaswende, Kisonono. · Kuumia kwa korodani, pengine inaweza kuwa chanzo ni ajali au michezo ya hatari, hali kama hiyo pia huweza kuchangia korodani kuvimba. · Maambukizi ya ‘epididymis’ ni chanzo kingine cha tatizo hili, ambapo ...