MAUMUVU WAKATI WA KUKOJOA NA TIBA

*Maumivu Wakati wa Kukojoa Yanavyotokea* Maumivu wakati wa kukojoa hutokana na kuchubuka kwa njia ya mkojo. Kuchubuka huku hutokea pale njia ya mkojo inaposhambuliwa na bakteria au kemikali na kuharibu ukuta wa juu wa njia ya mkojo hivyo huwa kama kidonda na wakati mwengine kuwa na kijiuvimbe kwenye njia ya mkojo. Pale mkojo unapopita eneo hili basi unapata maumivu kama ya kuungua. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wote unakojoa, mwanzoni au mwishoni mwa kukojoa. Kwa watoto wadogo, mara nyingi hulia wakati wanakojoa ikiwa wanapata maumivu kwani hawawezi kuongea. Pia yanaweza kuambatana na dalili nyingine kama homa, kutokwa na usaha au uchafu sehemu za siri, kutokwa mkojo wenye damu damu, maumivu chini ya kitovu au maumivu ya ubavu (flanks). *Sababu za Maumivu Haya* Maumivu haya hutegemea na chanzo cha ugonjwa unaoleta dalili hii. Baadhi ya vyanzo vya maumivu wakati wa kukojoa ni: *Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)* Ugonjwa huu huleta maumivu kama ya kuungua kw...