UGONJWA WA P.I.D (PELVICS INFLAMATORY DESEAS) DALILI,CHANZO,MADHARA NA MATIBABU

 


Wadada/Wanawake wanasumbuliwa sana huu ugonjwa ujumuishao magonjwa ya kizazi na via vyake pamoja na viungo vingine vinavoundwa kwa kulindwa na mifupa ya nyonga. 

P.I.D ni kifupi cha maneno ya Pelvic Inflammatory Disease yaani maambukizi katika kifuko cha kizazi cha mwanamke. Tunaposema mfumo wa uzazi tunamaanisha mji wa mimba ( mfuko wa uzazi ) mirija ya uzazi pamoja na viungo vya jirani.


P.I.D inasababishwa na maambukizi ya magonjwa ya  klamidia na kisonono pia bakteria wengine wanaweza kusababisha P.I.D wakati mwingine P.I.D husababishwa na bakteria zaidi ya aina moja.


KUFANYA HAYA KUNAKUWEKA KATIKA HALI YA HATARI ZAIDI KUPATA P.I.D 

>Kushiriki ngono na wapenzi wengi tofauti tofauti. 

>Kushiriki ngono na mwasirika wa magonjwa ya zinaa. 

>Kuchangia vifaa vya kuogea kama taulo

>Kuweka vitu vyenye kemikali ukeni kama vile sabuni, povu la sabuni, marashi.

>Kukaa na pedi 1 mda mrefu wakati wa hedhi. 

>Kua mchafu 

>Kubana mkojo kwa mda mrefu 

>Kujojisafisha vizuri hasa haja kubwa 

>Maradhi mengine kama U.T.I 

>Madhara ya vipandikizi na madawa ya kuzuia mimba.

>Kutoa mimba na mengine hatarishi kwa mfumo wa uzazi. 


Mwanamke / Mdada yeyote anaweza kupata P.I.D hata hivyo wanawake wenye umri kati ya miaka 13-35 hupata maambukizi Mara nyingi zaidi 


DALILI ZA P.I.D

Baadhi ya wanawake wenye maambukizi ya P.I.D hawana dalili zozote kama una dalili hizi unaweza kuwa na P.I.D 

■Kutoka uchafu mwingi, mweupe au njano,mzito kama maziwa mgando sehemu za siri

■Maumivu  ya mara kwa mara chini ya kitovu.

■Hedhi kuvurugika (Hedhi zisizoeleweka)

■Maumivu wakati wa kukojoa

■Maumivu wakati wa tendo la ndoa 

■Kutokwa na harufu mbaya ukeni

■Maumivu ya mara kwa mara nyonga ni


MADHARA YA  P.I.D

>Ugumba au utasa mwanamke anaweza kukosa uwezo wa kubeba mtoto kwa sababu ya P.I.D

>Mimba kutunga nje ya mfuko wa kizazi

>Maumivu sugu ya tumbo yaani chango la uzazi.

>Kuporomosha ujauzito 


UCHUNGUZI NA MATIBABU. 

Uchunguzi hufanyika katika vituo vya afya na hospitali. 

Baada ya daktari kukufanyia uchunguzi huo, atakuandikia dawa. P. I.D  inatibiwa kwa kutumia dawa za antibiotics, Dakatari anaweza kukupa dawa za vidonge au za sindano kadri atakavyoona inafaa. 

1. Metronidazole


2. ofloxacin,


3. levofloxacin,


4. ceftriaxone plus doxycycline, or


5. cefoxitin 


6. probenecid plus doxycycline. Metronidazol


Ikumbukwe ni vyema sana kama mwenza wako nae atachukua vipimo na kuanza matibabu. 


Kuna baadhi ya  wahanga hua dawa hizo wapewazo haziwasaidii hata kidogo au zinawasaidia kwa mda fulani alafu tatizo linajirudia tena. 

Katika hili ni kua makini na matumizi ya dozi kamili na kuepuka vitu vinavyoweza kuhatarisha kupata P.I.D tena Vinginevyo unaweza kua unatibu tatizo alafu unajihatarisha tena na tena.


Aidha, kwa ambao hawajajihatarisha na kupata ugonjwa huo tena lakini tatizo bado ni sugu licha ya kutumia dawa, ni vyema kutumia tiba mbadala kwa maana ya virutubisho lishe vyenye Ubora wa hali ya juu. 


Je, Umewahi kutumia  dawa mbalimbali za P.I.D na tatizo likaendelea kujirudia?

Wasiliana nami kwa msaada zaidi 

Piga simu

0684450076

Watsapp

0684450076


Comments

Popular posts from this blog

Madhra ya Punyeto Kwa Mwanaume

𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗨 π—­π—œπ—‘π—”π—­π—’ 𝗙𝗔𝗑𝗬𝗔 𝗠π—ͺπ—”π—‘π—”π—¨π— π—˜ π—”π—¦π—›π—œπ—‘π——π—ͺπ—˜ π—¦π—œπ— π—”π— π—œπ—¦π—›π—” π—©π—œπ—­π—¨π—₯π—œ π—¨π—¨π— π—˜

DALILI ZA HORMONE ZA KIUME ZILIZO ZIDI KWA MWANAMKE