FAHAMU UGONJWA WA P.I.D NA MATIBABU
🔻JE WAJUA NINI MAANA YA MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI? JIFUNZE SASA, SABABU, DALILI, MADHARA, NA TIBA 🔻
Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake.
▪️CERVIX hali ambayo hujulikana kama cervicitis,
▪️ ENDOMETRIUM kitabibu huitwa endometritis,
▪️ FALLOPIAN TUBES kitabibu kama salpingitis.
🔻 P. I. D HUSABABISHWA NA NINI? 🔻
Aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID,
▪️ Neisseria Gonorrhoeae
▪️Chlamydia trachomatis
ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.
Je mwanamke huambukizwaje PID?
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na
▪️Kufanya ngono isiyo salama
▪️Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
▪️Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
▪️Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
▪️Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
🔻DALILI ZA PID NI ZIPI 🔻
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
▪️ maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu
▪️Kupata maumivu ya mgongo
▪️Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. ▪️harufu mbaya sehemu za siri
▪️Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
▪️Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
▪️Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
▪️Kupata homa
🔻VIPIMO VYA PID🔻
Ili kuweza kutambua kama mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo
▪️Kuchunguza mkojo
▪️Kupima damu
▪️Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi
▪️Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.
🔻MATIBABU YA P. I. D🔻
Matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana na ugonjwa unaisha kirahis ikiwa umepata dose sahihi.
Piga simu sasa 0684450076
Comments