MIPASUKO KATIKA ULIMI

 TATIZO LA MIPASUKO KATIKA ULIMI


📚 Ulimi wa mtu kwa kawaida hautakiwi kuwa na mipasuko ya aina yoyote . Sasa hawa watu wenye ulimi uliopasuka huwa hawana maumivu , isipokua tu labda kama kuna chakula kimekwama kwenye hiyo mipasuko ndio muhusika atahisi maumivu


📚 Mipasuko hii huweza kuwa iliyochimbika sana au kiasi tu.

Wazee ndio hupatwa sana na hii mipasuko ya ulimi , japo yeyote yule anaweza kuwa na ulimi wa hivi.

Wanaume ndio huwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake


📤 NINI HUSABABISHA HALI HII ?


Hadi sasa , wataalamu hawajui ni nini hupelekea hali hii ya mipasuko kwenye ulimi , japo ina amini kwamba watu wenye undugu (genetics) huweza kuwa na tatizo hili na wengine wasiwe nalo . mfano katika familia , unaweza kuta mzazi ana tatizo hili na watoto pia

.

Mfano : Kuna tafiti ilifanyika na ikabaini kwamba watu wa South Africa ni 0.6% tu ya watu wote ndio wana tatizo hili la mipasuko kwenye ulimi , lakini Katika Taifa la Israel 30.6% ya watu wote ndio wana hii hali. Sasa unaweza ona kwamba swala la jamii fulani yenye mfanano wa kigenetiki huweza kuwa na hii hali ya mipasuko na jamii nyingine isiwe nayo


📤 TATIZO HILI LA MIPASUKO KATIKA ULIMI HUWA NA UHUSIANO NA MAMBO KAMA HAYA :


☂ Geographic tongue


☂ Kuvimba kwa lips na uso kutokana na matatizo ya neva

.

☂ Upungufu wa virutubisho muhimu kwa mwili n.k japo hii huwa na mchango mdogo


MATIBABU


Tatizo hili kiufupi , halihitaji tiba , isitoshe kisababishi hakijulikani , .


📤 USHAURI


Ubaya wa hii mipasuko ni kwamba endapo chakula kitabakia kwenye hiyo mipasuko , itapelekea bacteria kuzaliana , maumivu na hata kupelekea harufu mbaya ya kinywa na hata kuchangia meno kuharibika



Muhusika pia anakua katika mazingira marahisi ya kushambuliwa na fungus wa kinywa (candinda ablicans) , ikiwa imekutokea basi dawa zipo , onana na daktari sasa nikupe suruhisho la kudumu.



📚 Hakikisha unafanya usafi wa kinywa angalau mara mbili kila siku , na uwe na utaratibu wa kumuona daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka


Comments

Popular posts from this blog

MIPASUKO/MICHANIKO KWENYE ULIMI NA TIBA YAKE

KUVIMBA KWA KORODANI NA MAUMIVU YA KORODANI SABABU NA TIBA

ONDOA MSONGO WA MAWAZO NA REJESHA KUMBUKUMBU